OKWI NA NIYONZIMA KUIMALIZA YANGA




Kocha msaidizi wa Simba amesema anamatumaini ya kikosi chake kuibuka na ushindi mnono dhidi ya mahasimu wao Yanga katika pambano la Ngao ya Jamii 
 
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja, amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaifunga Yanga kesho na kutwaa taji la Ngao ya Jamii kama ambavyo wamekusudia.

Mayanja ameiambia SIMBA FC, mchezo dhidi ya Yanga,  utakuwa mgumu lakini kuwa na wachezaji wazoefu kwenye kikosi chao kama Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima, kunatamaliza mchezo huo mapema kwa wao kupata ushindi.

“Tunaingia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, tukijivunia Okwi na Niyonzima hata kama wasipofunga lakini uwepo wao ni ushindi tosha kwa Simba kwasababu asilimia kubwa ya wachezaji wa Yanga na mashabiki wao wanawaogopa wachezaji hao,”amesema  Mayanja.

Kocha huyo amesema wanakiu ya kushinda pambano hilo ili kuanza vyema msimu mpya wa ligi ya Vodacom na kubeba Ngao ya Jamii ni ishara nzuri kwao kwani kutawaongezea ari ya kucheza kwa kujituma na kutimiza kile ambacho wanakihitaji.

Pambano hilo la watani wa jadi linapigwa kesho uwanja wa Taifa Dar es Salaam, na Simba wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na aina ya wachezaji iliyowasajili msimu huu.

Comments

Popular posts from this blog

OKWI WE ACHA TU......

SIMBA HAITAJUTA KUNISAJILI