SIMBA HAITAJUTA KUNISAJILI
Gyan juzi alifungua akaunti yake ya magoli baada ya kufanikiwa kufunga goli moja dhidi ya Hard Rock kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Mghana huyo allifanya mahojiano na gazeti la Mwanaspoti alisema kiu yake ni kuona anafunga kila mechi.
“Baada ya kufanya vizuri katika ligi ya nyumbani Ghana, sasa nimekuja Simba ili kuendeleza kasi yangu ya ufungaji, Simba haitajuta kunisajili,” alisema hivyo Mghana huyo.
Gyan anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu wikendi hii dhidi ya Waoka mikatae wa Dar es salaam, Azam.
Comments
Post a Comment