OMOG""SIMBA MOTO ULE ULE
Kocha wa Simba amesema wamepania kuendeleza wimbi lao la ushindi katika michuano ya ligi kuu hivyo asingependa kutoa mapumziko kwa baadhi ya wachezaji Kocha mkuu wa Simba Joseph Omog amesema kikosi chake kitaendelea na mazoezi kwa wachezaji ambao hawapo timu ya Taifa lengo likiwa ni kulinda viwango vyao. Omog ameiambia SIMBA FC ameona afanye hivyo ili viwango vya wachezaji wake visishuke katika kiwango walichonacho kwa sasa ili waweze kuendeleza moto wao wakati ligi itakapoendelea Septema 5. "Tupo kwenye kiwango bora kwa sasa kuwapa wachezaji mapumziko ni sawa na kushusha viwango vyao na kupoteza ari ya kimchezo waliokuwa nayo hivi sasa hivyo ni bora tukaendelea na mazoezi mpaka Septemba 3 wakati kiksi kitakapokamilika," amesema Omog. Kocha huyo raia wa Cameroon amesema wamepania kuendeleza wimbi lao la ushindi katika michuano ya ligi kuu hivyo asingependa kutoa mapumziko kwa baadhi ya wachezaji ipi kutimiza kile walichokipanga. A...