OMOG""SIMBA MOTO ULE ULE
Omog ameiambia SIMBA FC ameona afanye hivyo ili viwango vya wachezaji wake visishuke katika kiwango walichonacho kwa sasa ili waweze kuendeleza moto wao wakati ligi itakapoendelea Septema 5.
"Tupo kwenye kiwango bora kwa sasa kuwapa wachezaji mapumziko ni sawa na kushusha viwango vyao na kupoteza ari ya kimchezo waliokuwa nayo hivi sasa hivyo ni bora tukaendelea na mazoezi mpaka Septemba 3 wakati kiksi kitakapokamilika," amesema Omog.
Kocha huyo raia wa Cameroon amesema wamepania kuendeleza wimbi lao la ushindi katika michuano ya ligi kuu hivyo asingependa kutoa mapumziko kwa baadhi ya wachezaji ipi kutimiza kile walichokipanga.
Amesema ligi ni ngumu kwa hivyo wanatakiwa kucheza kwa juhudi muda wote ili waweze kutwaa ubingwa kama walivyokusudia.
Simba ilianza kwa kishindo Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kuwafunga Ruvu Shooting mabao 7-0 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, jumamosi iliyopita.
Comments
Post a Comment