SIMBA HAINA HOFU KUCHEZA CHAMANZI
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja, amesema kucheza uwanja wa Chamaz ni nafasi kwa wachezaji wao kucheza bila msaada wa mashabiki Uongozi wa klabu ya Simba umesema hauhofii kitu chochote kuhusiana na Bodi ya Ligi kubadili ratiba na kuipanga mechi yao na Azam kupigwa uwanja wa Azam Complex Chamazi Jumamosi. Kocha msaidizi wa Simba Jackosn Mayanja, ameiambia SIMBA FC, ni mchezo mkubwa lakini kucheza uwanja wa Chamazi siyo kikwazo cha wao kushindwa kuendeleza kasi yao waliyoanza nayo. “Tunaheshimu maamuzi ya bodi ya ligi na Simba tumejipanga kuhakikisha tunashinda popote pale tunapocheza siyo uwanja wa Uhuru au Taifa peke yake nahiyo inatokana na ubora wa kikosi tulichonacho msimu huu,”amesema Mayanja. Kocha huyo amesema mabadiliko hayo yatawajenga wachezaji wao kucheza kwa kujituma bila sapoti ya karibu kutoka kwa mashabiki wao ambao wamekua wakijaa kwa wingi uwanjani kuwashangilia. Amesema kuna safari wanakwenda mikoani, hujikuta kama ...