SIMBA HAINA HOFU KUCHEZA CHAMANZI

Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja, amesema kucheza uwanja wa Chamaz ni nafasi kwa wachezaji wao kucheza bila msaada wa mashabiki 
 
Uongozi wa klabu ya Simba umesema hauhofii kitu chochote kuhusiana na Bodi ya Ligi kubadili ratiba na kuipanga mechi yao na Azam kupigwa uwanja wa Azam Complex Chamazi Jumamosi.
Kocha msaidizi wa Simba Jackosn Mayanja, ameiambia SIMBA FC, ni mchezo mkubwa lakini kucheza uwanja wa Chamazi siyo kikwazo cha wao kushindwa kuendeleza kasi yao waliyoanza nayo.

“Tunaheshimu maamuzi ya bodi ya ligi na Simba tumejipanga kuhakikisha tunashinda popote pale tunapocheza siyo uwanja wa Uhuru au Taifa peke yake nahiyo inatokana na ubora wa kikosi tulichonacho msimu huu,”amesema Mayanja.

Kocha huyo amesema mabadiliko hayo yatawajenga wachezaji wao kucheza kwa kujituma bila sapoti ya karibu kutoka kwa mashabiki wao ambao wamekua wakijaa kwa wingi uwanjani kuwashangilia.

Amesema kuna safari wanakwenda mikoani, hujikuta kama wanyonge kwa kukosa sapoti hivyo kucheza uwanja wa Chamazi msimu huu yeye anaamini kutakuwa na faida kwao ya kucheza bila kuhitaji sapoti ya mashabiki.

Ratiba iliyofanyiwa marekebisho ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, imetoka jana imeonyesha timu za Simba na Yanga ambazo zilikuwa hazichezi uwanja wa Azam Complex sasa kuanzia msimu huu zitakwenda kucheza huko pindi zinapopambana na wenyeji Azam FC.

Comments

Popular posts from this blog

OKWI NA NIYONZIMA KUIMALIZA YANGA

OKWI WE ACHA TU......

SIMBA HAITAJUTA KUNISAJILI