Posts

SIMBA HAINA HOFU KUCHEZA CHAMANZI

Image
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja, amesema kucheza uwanja wa Chamaz ni nafasi kwa wachezaji wao kucheza bila msaada wa mashabiki    Uongozi wa klabu ya Simba umesema hauhofii kitu chochote kuhusiana na Bodi ya Ligi kubadili ratiba na kuipanga mechi yao na Azam kupigwa uwanja wa Azam Complex Chamazi Jumamosi. Kocha msaidizi wa Simba Jackosn Mayanja, ameiambia SIMBA FC, ni mchezo mkubwa lakini kucheza uwanja wa Chamazi siyo kikwazo cha wao kushindwa kuendeleza kasi yao waliyoanza nayo. “Tunaheshimu maamuzi ya bodi ya ligi na Simba tumejipanga kuhakikisha tunashinda popote pale tunapocheza siyo uwanja wa Uhuru au Taifa peke yake nahiyo inatokana na ubora wa kikosi tulichonacho msimu huu,”amesema Mayanja. Kocha huyo amesema mabadiliko hayo yatawajenga wachezaji wao kucheza kwa kujituma bila sapoti ya karibu kutoka kwa mashabiki wao ambao wamekua wakijaa kwa wingi uwanjani kuwashangilia. Amesema kuna safari wanakwenda mikoani, hujikuta kama ...

SIMBA HAITAJUTA KUNISAJILI

Image
Kwa namna Gyan alivyoonyesha uwezo, ni lazima wapangue safu ya ushambuliaji na kuunda kombinesheni mpya kwa mujibu wa Jackson Mayanja    Mshambuliaji mpya wa Simba raia wa Ghana, Nicholas Gyan, aliyesajiliwa msimu huu akitokea klabu ya Ebusua Dwarfs ya Ligi Kuu Ghana amesema atahakikisha ana funga kila mechi atakayopewa nafasi na mwalimu. Gyan juzi alifungua akaunti yake ya magoli baada ya kufanikiwa kufunga goli moja dhidi ya Hard Rock kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Mghana huyo allifanya mahojiano na gazeti la Mwanaspoti alisema kiu yake ni kuona anafunga kila mechi. “Baada ya kufanya vizuri katika ligi ya nyumbani Ghana, sasa nimekuja Simba ili kuendeleza kasi yangu ya ufungaji, Simba haitajuta kunisajili,” alisema hivyo Mghana huyo. Gyan anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu wikendi hii dhidi ya Waoka mikatae wa Dar es salaam, Azam.

AZAM FC YAFURAHIA MECHI ZAKE NA SIMBA KUPELEKWA CHAMANZI

Image
Mabadiliko ya ratiba mpya ya Ligi Kuu yanaonyesha kuwa mechi zote za Azam FC za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zitafanyika Uwanja wa Azam Complex.   Klabu ya Azam FC imefuraishwa na taarifa za shirikisho la mpira TFF kuruhusu mechi zao dhidi ya  Simba na Yanga kufanyika kwenye uwanja wao wa Chamanzi. Kwa mara ya kwanza mechi ya Azam na Simba itafanyika katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi hii Septemba 9. " Ni furaha tupu ndani ya viunga vya Azam Complex kwenye makao makuu ya Klabu BIngwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuiruhusu timu hiyo kutumia uwanja huo kwa mara ya kwanza kwenye mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga. waliandika hivyo kupitia kwenye mtandao wao wa klabu.

OMOG""SIMBA MOTO ULE ULE

Image
Kocha wa Simba amesema wamepania kuendeleza wimbi lao la ushindi katika michuano ya ligi kuu hivyo asingependa kutoa mapumziko kwa baadhi ya wachezaji    Kocha mkuu wa Simba Joseph Omog amesema kikosi chake kitaendelea na mazoezi kwa wachezaji ambao hawapo timu ya Taifa lengo likiwa ni kulinda viwango vyao. Omog ameiambia SIMBA FC ameona afanye hivyo ili viwango vya wachezaji wake visishuke katika kiwango walichonacho kwa sasa ili waweze kuendeleza moto wao wakati ligi itakapoendelea Septema 5. "Tupo kwenye kiwango bora kwa sasa kuwapa wachezaji mapumziko ni sawa na kushusha viwango vyao na kupoteza ari ya kimchezo waliokuwa nayo hivi sasa hivyo ni bora tukaendelea na mazoezi  mpaka Septemba 3 wakati kiksi kitakapokamilika," amesema Omog. Kocha huyo raia wa Cameroon amesema wamepania kuendeleza wimbi lao la ushindi katika michuano ya ligi kuu hivyo asingependa kutoa mapumziko kwa baadhi ya wachezaji ipi kutimiza kile walichokipanga. A...

OKWI WE ACHA TU......

Image
Simba wameonyesha ishara njema ya kupata mafanikio Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kuanza ligi kwa ushindi wa mabao 7 Emmanuel Okwi akiongeza sherehe.   Simba SC imeanza Ligi Kuu Bara na moto mkali, baada ya kuichapa mabao 7-0 Ruvu Shooting jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi ameonyesha msimu huu amedhamiria kurudi kivingine katika Ligi Kuu, baada ya kufunga mabao manne na kuseti moja katika ushindi huo mnono. Mabao mengine ya Wekundu wa Msimbazi, walio chini ya kocha Mkameruni, Joseph Marius Omog anayesaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja yamefungwa na Shiza Ramadhani Kichuya, Juma Luizio Ndanda na Erasto Edward Nyoni. Okwi alifungua sherehe za mabao dakika ya 18 akimchambua kipa Bidii Hussein baada ya pasi ya Muzamil Yassin na bao la pili akafunga dakika ya 22 baada ya kuwachambua mabeki ndani ya boksi kufuatia pasi ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima. Okwi akakamilisha hat trick yake dakik...

OKWI NA NIYONZIMA KUIMALIZA YANGA

Image
Kocha msaidizi wa Simba amesema anamatumaini ya kikosi chake kuibuka na ushindi mnono dhidi ya mahasimu wao Yanga katika pambano la Ngao ya Jamii    Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja, amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaifunga Yanga kesho na kutwaa taji la Ngao ya Jamii kama ambavyo wamekusudia. Mayanja ameiambia SIMBA FC, mchezo dhidi ya Yanga,  utakuwa mgumu lakini kuwa na wachezaji wazoefu kwenye kikosi chao kama Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima, kunatamaliza mchezo huo mapema kwa wao kupata ushindi. “Tunaingia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, tukijivunia Okwi na Niyonzima hata kama wasipofunga lakini uwepo wao ni ushindi tosha kwa Simba kwasababu asilimia kubwa ya wachezaji wa Yanga na mashabiki wao wanawaogopa wachezaji hao,”amesema  Mayanja. Kocha huyo amesema wanakiu ya kushinda pambano hilo ili kuanza vyema msimu mpya wa ligi ya Vodacom na kubeba Ngao ya Jamii ni ishara nzuri kwao kwani kutawaongezea ari ya k...

MACHO YOTE KWA NIYONZIMA NA AJIBU

Image
Pambano lililosubiriwa kwa siku nyingi limefika, ni Simba dhidi ya Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii, Niyonzima na Ajibu wakikabili timu zao za kale    Miamba ya soka Tanzania Yanga na Simba inakutana kesho Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii ambao unaashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom. Presha imekuwa kubwa kwa pande zote mbili, huku Simba wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na usajili ambao wameufanya msimu huu kwa kusajili nyota wenye majina makubwa. Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa ni Februari mwaka huu, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, kwahiyo usajili walioufanya msimu huu pamoja na ushindi walioupata mwisho kumewajengea imani mashabiki wa Simba wakiamini rekodi hiyo itaendelea tena kesho. Kuelekea mchezo huo Yanga wameendelea kujifua kwa kutumia nyota waliosajili kipindi hiki cha usajili ingawa mashabiki wao wameonyesha hofu kutokana na u...