MACHO YOTE KWA NIYONZIMA NA AJIBU
Presha imekuwa kubwa kwa pande zote mbili, huku Simba wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na usajili ambao wameufanya msimu huu kwa kusajili nyota wenye majina makubwa.
Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa ni Februari mwaka huu, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, kwahiyo usajili walioufanya msimu huu pamoja na ushindi walioupata mwisho kumewajengea imani mashabiki wa Simba wakiamini rekodi hiyo itaendelea tena kesho.
Kuelekea mchezo huo Yanga wameendelea kujifua kwa kutumia nyota waliosajili kipindi hiki cha usajili ingawa mashabiki wao wameonyesha hofu kutokana na uwepo wa Emmanuel Okwi na kiungo Haruna Niyonzima aliyekuwa kwenye kikosi chao msimu uliopita.
Timu zote mbili zilipiga kambi Visiwani Zanzibar, zikijiandaa na mchezo huo maalumu na kila timu imeweza kucheza mechi za kirafiki kuvipima vikosi vyao kabla ya mchezo huo.
Yanga wamecheza mechi nne mbili Dar es Salaam na mbili Zanzibar ambapo kati ya hizo imeshinda tatu na kupoteza moja wakati Simba imecheza mechi sita imeshinda tatu imetoka sare mbili na kufungwa mchezo mmoja.
Kwa tathimini ukiangalia viwango vya timu zote mbili Simba licha ya kusajili wachezaji wenye majina makubwa, lakini timu yao imeonakana kuwa na mapungufu kwenye umaliziaji kwani katika mechi sita walizocheza wameweza kufunga mabao nane mchezo wa mwisho dhidi ya Gulioni wakifunga mabao matano tofauti na mechi nyingi tano ambazo walikuwa wakipata ushindi hafifu wa bao 1-0.
Yanga wao katika mechi yao ya kwanza ya kirafiki waliifunga Moro Kids mabao 5-0, kisha wakaifunga Singida United mabao 3-2, na baadaye wakafungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting.
Walipokwenda Zanzibar wakaifunga Mlandege mabao 2-0 kabla ya kumaliza na Jamhuri ambayo waliifunga bao 1-0.
Takwimu hizo zinaonyesha namna safu ya ulinzi ya Simba ilivyokuwa imara kwa kuruhusu mabao mawili katika mechi zita walizocheza lakini safu yao ya ushambuliaji imeshndwa kufanya vizuri licha ya uwepo wa John Bocco, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya, Laudi Mavugo na Mohamed Ibrahim.
Pamoja na yote kitakachoamuamchezo wa kesho ni eneo la kiungo ambalo mara nyingi Simba wamekuwa wakilitawala na kuwapoteza Yanga, Simba imekuwa na tabia ya kujaza viungo wengi na kuwameza viongo wa Yanga kitu kinachosababisha wautawale mchezo na kufanya mashambulizi mengi.
Mbinu za kila kocha ndiyo zinazoweza kuamua mshindi wa mchezo huo, kwasababu kila kocha amekuwa na mbinu mbadala ambazo zinaweza kumsaidia kupata matokeo katika mchezo huo muhimu.
Kocha George Lwandamina ataendelea kuwategemea Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Ibrahim Ajibu, Thabani Kamusoko na Papy Kabamba Tshishimbi na kipa Youth Rostand ambao wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.
Lwandamina mtaalamu wa mfumo wa 4-3-3, anatazamiw kufanya maajabu ili kukifunga kikosi kilicho garimu kiasi cha Bilioni 1-3, kwenye usajili wake msimu huu.
Kocha wa Simba Joseph Omog mtaalam wa mfumo wa 4-4-2 niwazi ataingia kwenye mchezo huo akiwa na hamu ya kutaka kupata ushindi ili kuwadhihirishia mashabiki wake kile ambacho amekuwa akikiwaza nacho ni ubingwa.
Aishi Manula bila shaka ndiye atakayeanza langoni akisaidiwa na Mohamed Husseni, Erasto Nyoni ingizo jipya atakuwa upande wa kulia wakati kati atakuwepo Salum Mbonde na Method Mwanjali.
Kiungo mkabaji ataanza James Kotei, Shiza Kichuya, Haruna Niyonzima , Mohamed Ibrahim John Bocco na Emmenuel Okwi

Comments
Post a Comment