AZAM FC YAFURAHIA MECHI ZAKE NA SIMBA KUPELEKWA CHAMANZI
Kwa mara ya kwanza mechi ya Azam na Simba itafanyika katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi hii Septemba 9.
" Ni furaha tupu ndani ya viunga vya Azam Complex kwenye makao makuu ya Klabu BIngwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuiruhusu timu hiyo kutumia uwanja huo kwa mara ya kwanza kwenye mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga. waliandika hivyo kupitia kwenye mtandao wao wa klabu.
Comments
Post a Comment